Bila
shaka sasa wamedhamiria kurudisha heshima yao iliyopotea kwa miaka
mitatu baada ya kushindwa kushika nafasi mbili za juu na kujikuta
wakikosa kuwakilisha nchi katika michuano mikubwa barani Afrika.
Katika miaka yote hiyo, Simba wamewaachia Yanga na Azam FC wakitamba anga za kimataifa.
kwa mara ya mwisho Simba kutwaa ubingwa ni mwaka 2012 chini ya kocha Mserbia, Milovan Circovic.
Msimu
uliopita, Simba ilishika nafasi ya nne ikifundishwa na Goran Kopunovic,
lakini msimu ujao inaonekana wamedhamiria kufanya vizuri.
Kwa
muda wa wiki kadhaa waliweka kambi Lushoto, Tanga kabla ya kupanda Boti
na kutua visiwani Zanzibar ambako wana utamaduni wa kwenda mara kwa
mara.
Kikosi
hicho kinaendelea kujifua uwanja wa Amaan Zanzibar chini ya Muingereza,
Dylan Kerr ambaye dhahiri anaonekana kuwa na hamu ya kurudisha heshima
ya Simba.
0 comments:
Post a Comment