Timu ya Simba leo imepewa mapuziko ya siku moja kwa ajili ya kuupumzisha mwili kabla ya kesho saa 2 asubuhi kuchanya mazoezi ya viungo tayari kwa kuikabili timu ya Zanzibar Combain katika uwanja wa Amani Zanzibar saa 11 jioni.
Simbasports.co.tz ilipata nafasi ya kuongea na kocha mkuu wa timu ya Simba Dylan Kerr na kusema haya “Mechi ya kesho itakuwa ni kipimo kizuri sana katika timu yangu ya Simba kujitayarisha na mechi kubwa kati ya Simba na AFC Leopards ya kutoka nchini Kenya katika siku ya Simba Day. Tunategemea kufanya vizuri katika mchezo wa kesho na si Kesho tu bali hata kwenye mechi yetu kubwa ya kwanza na AFC Leopards”.
Kama ilivyoelezwa hapo awali timu ya Simba itaikabili timu ya AFC Leopards kutoka Kenya siku ya Simba Day tarehe 8 – 8 – 2015 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, na kwa walio na kadi mpya za uanachama wa Simba wataingia bure kwenye mechi hiyo.
Simbasports.co.tz itakuletea matokeo ya mchezo huo wa kwanza wa kirafiki tangu wafike katika kambi ya visiwani Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment