JAMAA AKISAFISHA BAADA YA KUBAMBWA NA WADAU UWANJA WA TAIFA, LEO.Ukishangaa ya Musa, utayaona ya Firauni! Hivi watu bado wanajisaidia haja ndogo kwenye sinki zinazotumika kunawia mikono au uso? |
Imetokea
leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati Yanga ikiivaa Al
Kharthoum ya Sudan.
Jamaa
mmoja, amewahi kuingia chooni na kwenda kuanza kujisaidia haja ndogo kwenye
sinki hizo kwa ajili ya kunawia.
Mashabiki
walioingia chooni, wakamnasa. Acha wamkomalie, wengine wakitaka kumpiga,
wengine watakata kumywesha mkojo wake.
Akionekana
amechanganyikiwa, jamaa alianza kujitetea akisema: “mimi nilidhani choo cha
wanawake ndiyo wanatumia hivyo.”
Jibu
lake lilionekana kuwaudhi zaidi wakawa wanataka kumpiga, wengine waliojitokeza
na kuwapoza wenzao kuwa na jazba na kuwataka wampe adhabu ya kufanya usafi.
Ndipo
aliposimamiwa na kuanza kufanya usajifi wa sinki moja baada ya jingine.
Mtu
huyo wa ajabu kabisa aliyewashangaza wengi, alionekana ana umri takribani miaka
45 hivi, lakini anajisaidia kwenye sinki!
0 comments:
Post a Comment