SIMBA imezidi kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo jana Kocha Mkuu wa timu hiyo, Dylan Kerr, aliendelea kuwapima wachezaji wake katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Black Sailory ya Zanzibar.
Simba waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 na waliocheka na nyavu ni Elius Maguli, Maganga, Abdi Banda na Hassan Isihaka
Kikosi chicho ambacho kimeweka kambi ya wiki mbili Mjini Unguja, kimeendelea kuiva ili huku kocha wake Kerr akiwapa wachezaji wake mbinu mbalimbali na kuwajengea stamina kabla ya Ligi Kuu Bara kuanza.
Kerr anatarajia kuunda kikosi cha kwanza ambacho kitacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya FC Leopards ya Kenya utakaopigwa Agosti 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

0 comments:
Post a Comment