MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

BOBAN HUYOOO OMAN, AJARIBU TENA BAHATI YAKE


Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Haruna Moshi ‘Boban’, anajaribu tena bahati yake ya kucheza soka la kulipwa, baada ya kutimkia nchini Oman kufanya majaribio lakini kuna taarifa nyingine inafafanua kuhusu jinsi Mbeya City ilivyomkosa kiungo huyo dakika za mwisho.


Miaka kadhaa iliyopita, Boban alikuwa akiichezea Gefle IF inayoshiriki Ligi Kuu ya Sweden lakini alishindwa kuelewana na kocha wale, Perre Olson ambaye baadaye alitaka abaki lakini akashindwa kumshawishi Boban ambaye alirejea nchini na baadaye kujiunga na Coastal Union baada ya kukaa msimu mzia bila kucheza.


Inadaiwa kuwa Boban ameshamaliza wiki sasa tangu atimkie zake nchini humo kusaka bahati kwa mara nyingine.

Herry Mzozo ambaye ni kocha wa Friends Rangers ya Ligi Daraja la Kwanza inayommiliki mchezaji huyo, amesema:

 “Boban ameondoka, yupo Oman kwa muda wa wiki sasa. Kuna timu imemuita ambayo itatajwa baada ya kumalizana kila kitu. Mbeya City walionyesha nia ya kumtaka tangu mwanzo lakini sijui ilikuwaje baadaye wakawa kimya.


“Sasa walirejea hivi karibuni kuonyesha kuwa wanamhitaji na wamejikamilisha lakini ikawa wameshachelewa, mipango ya Boban ilikuwa imeshakaa sawa, kwa hiyo wakawa wamepishana naye lakini pengine wangekuwa na maamuzi tangu mwanzo, wangeweza kumchukua,”  alifafanua Mzozo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment