Akiongea wakati wa kukabithi hundi za malipo kwa wachezaji hao, Rais wa Simba Evans Aveva alisema ” wakati tunaingia madarakani tuliahidi kusaidia wachezaji wetu wa Zamani kujiendeleza hususani kwenye ukocha, hawa ni Watu muhimu mno kwa timu yetu na walitoa mchango mkubwa kwa timu yetu. Uongozi wangu utaendelea kutekeleza kwa vitendo ahadi za wakati wa uchaguzi”.
Simbasports.co.tz inapenda kuwapongeza Suleiman Matola, George Lucas “Gaza” na Yusuf Macho “Musso” kwa kuamua kujiendeleza kwenye taaluma ya ukocha, Kwani ujuzi na uzoefu wao wa uchezaji Mpira utakuwa chachu kubwa kuwa makocha wazuri na kuendeleza soka Nchini Tanzania.
0 comments:
Post a Comment