LOGA |
Kocha Mkuu wa FC Leopards ya Kenya, Zdravko Logarusic amesema kipa Ivo Mapunda, hatasajiliwa na kikosi chake kwa ajili ya msimu huu.
Logarusic amesema amemualika Ivo kwenda Kenya kujumuika na kikosi chake ambako atakuwa akifanya mazoezi ili kujiweka imara.
“Baada ya hapo, atarejea Dar es Salaam hasa baada ya kumalizika kwa ligi. Sasa zimebaki mechi chache ligi isimame.
“Hakuna suala la usajili, hivyo Ivo atakuwa nasi hadi ligi itakapoisha na baada ya usajili kuanza, basi tutazungumza naye ili aanze kazi rasmi,” alisema ambaye sasa ameanza likizo fupi.
Ivo ameachwa na Simba baada ya uongozi wa klabu hiyo kusema alikuwa msumbufu akishindwa kutokea kumalizana nao licha ya kwamba walishampa fedha za usajili.
Simba iliamua kumsajili kipa kutoka Ivory Coast na sasa inamuwinga kipa wa JKU ili kujiimarisha zaidi.
0 comments:
Post a Comment