Kiungo aliyewahi kuifunga Yanga bonge la bao wakati akiwa Azam FC, Joseph Kimwaga ambaye hivi karibuni alitua Simba kwa mkopo, amefunguka kuwa Msimbazi pagumu na ana kazi kubwa ya kupata namba katika kikosi hicho cha Muingereza, Dylan Kerr.
Kiungo huyo ametua Simba hivi karibuni kwa mkopo wa mwaka mmoja, baada ya kuwa nje ya uwanja kwa msimu mzima kutokana na kuandamwa na majeraha akiwa Azam.
Tayari Klabu ya Simba ina viungo kadhaa kama Awadhi Juma, Peter Mwalyanzi na Justice Majabvi.
Kiungo huyo alisema kuwa kwa sasa ana mtihani mkubwa kuhakikisha kuwa anafanya kweli msimu ujao, japo bado ushindani ni mkubwa.
“Si kazi rahisi iliyopo mbele yangu, hasa kwa kuhakikisha napambana ili kuweza kupata namba kwa sababu juhudi zangu ndizo zitaweza kunipa nafasi ya kuweza kuwa kikosi cha kwanza.
“Pia natakiwa kuzingatia yale ambayo kocha anatuelekeza na Mungu aniepushe na majeraha ili niweze kufanya vyema msimu ujao ambao ni wazi ushindani wa namba na ligi kwa ujumla ni mgumu,” alisema Kimwaga.
Ikumbukwe kuwa, kiungo huyo aliifunga Yanga bao kali la shuti msimu wa 2013/14 ukiwa ni mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ambao Azam FC ilishinda 3-2.
0 comments:
Post a Comment