Pamoja na kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi chake cha Royal Eagles cha Afrika Kusini, kiungo mwenye kasi, Uhuru Selemani amekuwa akiendelea kujifua kwa nguvu.
Wakati wenzake wamepumzika, Uhuru ameendelea kujifua kwenye gym nchini Afirka Kusini. Lakini kiburudisho ni kwamba anajifua akiwa amevaa jezi ya Simba.
Uhuru amejiunga na timu hiyo kwa mkopo akitokea Jomo Cosmo ambayo imemsajili kutoka Mwadui FC. Kabla ya hapo, Uhuru alikuwa akikipiga Simba.
Wakati wenzake wamepumzika, Uhuru ameendelea kujifua kwenye gym nchini Afirka Kusini. Lakini kiburudisho ni kwamba anajifua akiwa amevaa jezi ya Simba.
Baada ya kuzipata picha hizo, SIMBA DUME-TEMBONI ilimsaka Uhuru ambaye yuko jijini Darbun na kutaka kujua kulikoni.
“Kweli, nimekuwa nikifanya sana mazoezi binafsi kwa kuwa ninataka kufikia malengo.
“Kuhusu jezi ya Simba, nimekuwa nikifanya nayo mazoezi hasa mazoezi ya peke yangu, sioni kama ni tatizo,” alisema Uhuru.
Bado klabu yake inapambana kupata kibali cha kazi ili kumruhusu acheze soka nchini humo.
Uhuru amejiunga na timu hiyo kwa mkopo akitokea Jomo Cosmo ambayo imemsajili kutoka Mwadui FC. Kabla ya hapo, Uhuru alikuwa akikipiga Simba.
0 comments:
Post a Comment