Golikipa mkongwe katika soka la Tanzania ambaye amecheza kwa kiwango cha juu kwa muda mrefu Juma Kaseja amerejea tena katika soka baada ya kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi sita. Kaseja amerejea uwanjani na amesajiliwa na klabu ya Mbeya Cityhivyo msimu ujao tutamuona langoni.
Katika maandalizi ya kurudi langoni Kaseja ametengeneza viatu maalum kwa ajili yake hivyo usishangae kumuona akiwa langoni na viatu vyenye jina lake Kaseja Coper 1pamoja na gloves. Kaseja ametoa exclusive hiyo kwa millardayo.com ila amegoma kutaja gharama ya aliotumia kutengeneza viatu hivyo.
Kaseja ambaye amewahi kupatiwa jina la Tanzania One kutokana na umahiri wake awapo langoni Je ni mpango wake kufanya biashara ya vifaa vya michezo kwa kutumia jina lake jibu ni kuwa ametengeneza kwa ajili yake pekee.
0 comments:
Post a Comment