Hi
Miaka 35 iliopita nikiwa na umri mdogo sana. Wakati huo nikisoma nursery kwenye skuli ya Tanganyika... Nna kumbukumbu ya nusunusu juu ya pengine mchezo wangu rasmi wa kwanza kushuhudia wa timu ya taifa ya Tanzania ambayo ilikuwa ikicheza na nchi ya Nigeria (Green Eagle's).
Nimeita kumbukumbu nusunusu sababu ya umri mdogo niliokuwa nao wakati huo. Lakini ktk nusu nnazozikumbuka. Nilipanda basi la timu ya taifa ambalo kama sikosei those dayz FAT (sasa tff) walikuwa wanalimiliki.
STARS INAENDELEA KUJIFUA NCHINI UTURUKI |
Nakumbuka timu iliondokea hoteli ya Africana na sisi tulikuwa kule for weekend na mzee ambaye inawezekana alinipigia pande kupanda basi la mashujaa wale ambao kwangu sitawasahau kamwe.
Nnazo kumbukumbu pia bendi ya DDC Mlimani Park ilitumbuiza kabla na wakati wa mapumziko katika mechi ile murua kabisa. Ingawa kwa siku zile sikujua kama wale ndio sikinde ngoma ya ukae!
Nusunusu yangu inanikumbusha kikosi kilichoanza game ile.
1-Juma Pondamali
2-Leopard Tasso Mukebezi
3-Hasan Zito Kiaratu
4-Jellah Mtagwa(C)
5-Ishaka Hassan Chukwu
6-Salim Amiri
7-Omari Hussein
8-Mohammed Rishard Adolph
9-Peter Tino
10-Mohammed Salum
11-Thuweni Ally
Kocha Mkuu alikuwa Joel Nkaya Bendera,
kwangu hii timu ambayo ilitoka kucheza fainali za mashindano ya Mataifa huru ya Afrika (Afcon) ilikuwa timu bora ya taifa kuwahi kuiona ingawa nilikuwa nusu mtu!
Timu hii ilimkosa nahodha wake mkuu Leodgar Chillah Tenga ambaye alikuwa ameumia kwenye mchezo wa liliokuwa kombe maarufu siku hzo likiitwa Jengo Cup ambapo timu yake ya pan African ilicheza na yanga.
Bahati mbaya hyo ndiyo ilikuwa game ya mwisho rasmi kwa tenga ambaye aljeruhiwa vbaya sana goti na baba yangu mkubwa Kitwana Manara ‘Popat’.
Ifahamike hyo ilikuwa mechi ya mechi ya marudiano dhidi ya Maafrica Magharibi hao ambapo kwenye game ya kwanza kule Surulele Stadium Nigeria tulitoka suluhu bin suluhu.
Bahati mbaya kwetu wakatufunga mbili mtungi huku ikitajwa kukosekana kwa tenga kuliififisha defence line ya Stars. Siku hiyo alitumika defender chipukizi(wakati huo) Chukwu ambaye ndiye aliyeziba pengo la captain Tenga
Iwapo kama tungefanikiwa kuwatoa wala pilipili wale. Stars ilikuwa ikutane na Algeria ambao ndio waliofuzu kucheza Kombe la Dunia la Spain 1982,
Mungu jalia bahati haikuwa yetu. Lakini tulikuwa karibu kabisa na World Cup kuliko kipindi chochote cha uhai wa taifa hili!
Katika miaka yake yote ya uhai wa mataifa yetu mawili. Nchi hizi zmekutana mara tatu tu. Ukiacha game hizo za kufuzu kwa Kombe la Dunia. Stars na mwewe hawa washawahi kukutana pia kwenye mechi ya ufunguzi wa Kombe la Mataifa huru ya Africa (Afcon) pale Lagos na Stars tukalala 3-1.
Miaka ya mwishon mwa miaka ya 1990 tulicheza nao lakini ilikuwa kwenye mechi ya kufuzu kwa michezo ya Olimpiki ambayo wachezaji wanaoruhisiwa kucheza ni wale walio chini ya miaka 23.
Mechi hizi pia wapo hao walitutoa na nakumbuka walikuja na nyota wao Tijan Babangida ambaye ni ndugu wa winga mahiri wa zamani wa ajax Amsterdam.
Nimeandika waraka huu mrefu kdogo ili itukumbushe shughuli tuliyo nayo mbeleni. Kwanza kihistoria baina yetu, pili kiuhalisia kuhusu uwezo wa kabumbu wa wapinzani wetu hawa ambao wamejaaliwa mamia ya wanasoka wanaocheza soka huko Ulaya.
Najua kwenye mpira lolote linawezekana. But tuendelee na maandalizi yetu huku tukiomba kwa Mungu pia, na hasa kheri tunaweza kuishangaza Afrika kwa kuwafunga manguli hawa wa kandanda si Afrika tu bali ulimwenguni kote.
Nimalizie kwa kuwataka radhi kwa errors mbili tatu.na kuwaomba sote kwa pamoja tuweke silaha chini kwa interest ya taifa letu
Mungu ibariki Stars
Mungu ibariki Tanzania
Amiin
Haji S.Manara
0 comments:
Post a Comment