Bao
pekee la Awadh Juma limetosha kuipa ushindi klabu ya Simba dhidi ya SC
Villa ya Uganda katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyomalizika
jioni ya leo uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Awadh
amecheka na nyavu dakika ya 90 na kuwapa raha mashabiki wa klabu hiyo
waliofurika kwenye mtanange huo kwa kuadhaminisha siku ya Simba, 'Simba
Day".
Hii
ni mara ya kwanza kwa Simba kushinda mechi ya Simba Day tangu ianzishwe
mwaka 2008 chini ya mwenyekiti Hassan Dalali akishirikiana na msaidizi
wake, Omar Gumbo.
0 comments:
Post a Comment