MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

CHEKI RAIS AVEVA ALIVYOZINDUA TAWI LA SIMBA DUME-TEMBONI


Kikosi cha Simba cha rejea
Kikosi cha Simba Sports Club leo kimewasili jijini Dar es salaam kikitokea Zanzibar kilipokuwa kimekita kambi yake kwa ajili ya matayarisho ya mechi yake ya kimataifa siku ya Simba Day pamoja na kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara.
Simba imerudi leo saa 5 asubuhi ikiwa na kikosi kamili cha Simba kikiongozwa na kocha mkuu Dylan Kerr pamoja na kocha msaidizi Suleiman Matola. Wakiwa Ferri jijini Dar es Salaam, simbasports.co.tz ilipata nafasi ya kuongea na kocha mkuu wa Simba Dylan Kerr nakusema “kambi yetu ilikuwa nzuri sana, hali ya hewa ya Zanzibar ilikuwa nzuri sana hasa kwa mafunzo tuliyokuwa tunayatoa kwa timu yetu, tumerudi leo na matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mechi yetu ya ya kwanza ya kimataifa pamoja na msimu mzima wa ligi kuu ya Vodacom”.
Kikosi cha Simba leo kilishiriki katika matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushiriki katika uzinduzi wa tawi jipya la Simba Dume Temboni Kimara jijini Dar es Salaam na baadae kutembelea kampuni ya TBL.
Simba Sports Club imerejea ikiwa na historia ya kutopoteza mchezo hata mmoja katika mechi zake zote za majaribio walizocheza wakiwa visiwani Zanzibar.
Kikosi cha Simba kitakutana na Sports Club Villa ya Uganda uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika siku ya Simba Day tarehe 8 – 8 – 2015.
Simbasports.co.tz itaendelea kukuletea taarifa na matukio yote yatakayo kuwa yakifanya na timu zote za Simba na Sports Club Villa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment