Simbasports.co.tz iliongea na kaimu katibu mkuu wa Simba Collin Frisch ambaye alisema kuwa wameamua kuwasajili wachezaji hao baada ya benchi la ufundi la Simba kuridhishwa na kiwango walichoonesha wachezaji hao katika kipindi ambacho walikuwa wakifanyiwa majaribio.
Kikosi cha Simba kwa sasa kipo visiwani Zanzibar katika muendelezo wa matayarisho ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara 2015/2016.
Simbasports.co.tz itaendelea kukuletea habari kuhusu kikosi cha Simba kilichopo visiwani Zanzibar kadiri zinavyoendelea kupatikana. SIMBA NGUVU MOJA
0 comments:
Post a Comment