MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

Aveva afungua tawi jipya la Simba Damu Fans

Aveva afungua tawi jipya la Simba Damu Fans
Katika muendelezo wa kuongeza wigo wa wanachama uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wa Simba Evance Aveva umezindua tawi jipya la wanachama SIMBA DAMU FANS Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam. Akizindua tawi hilo jijini Dar es Salaam Rais wa Simba Evans Aveva alisema “kama ilivyokuwa katika ahadi zetu kipindi cha uchaguzi uongozi umeazimia kufikisha jumla ya wanachma 50,000 kutoka wanachama wasiozidi 3,000. Hii sio kazi rahisi lakini kwa kushirikiana kwa pamoja tunaweza kama kauli mbiu yetu inavyotukumbusha SIMBA NGUVU MOJA”
Leo nipo hapa kwenu nikizindua tawi jipya la SIMBA DAMU FANS ni matarajio yangu kuwa litakuwa chachu ya ushindi wetu msimu huu kwani kama tunavyojua kuwa ushangiliaji ni sehemu kubwa sana katika kutafuta ushindi. Pamoja na hilo kama ambavyo tunafahamu kuwa wanachama wote wenye kadi mpya ya Simba situ wanakuwa wanachama bali kadi mpya hizi za Simba zinakuwezesha kupata bima ya maisha mpaka TSh 250,000 pindi mwenza wako, mtoto wako au Mwanachama mwenyewe akifariki, Alisema Rais Evans Aveva.
Simbadumetemboni.blogspot.com inawapongeza wanachama na wapenzi wa Simba kwa kufungua tawi jipya la SIMBA DAMU FANS kwa maendeleo ya Simba.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment