Kiungo wa Simba, Jonas Mkude aliungana na wachezaji wenzake mazoezini na ilipofikia wakati wa kupiga push up, tayari ikazua mjadala.
Mjadala ulianza hivi; wakati anapiga mazoezi ya push up, ile aina ya upigaji wake push up uliwavutia wengi kwa kuwa alikuwa akitumia mkono mmoja.
Lakini wengi wakaanza kukumbuka yale mambo ya Mgombea wa Urais wa CCM, John Pombe Magufuli ambaye amekuwa akipiga push up.
Baadhi ya mashabiki waliokuwa uwanjani pale walianza kutania kuwa alikuwa ana “Magufulika” kwa aina yake.
Simba iliendelea na mazoezi kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment