picha zote na Ben Shija...
Familia ya Mzee Ally Samatta leo ilikuwepo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kumpokea na kumpongeza mtoto wao Mbwana Samatta kwa mafanio makubwa aliyoyapata kwenye soka kwa kutwaa ubingwa wa Afrika pamoja na kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo kwa mwaka huu.
Mzee Ally Samatta ambaye alikuwa ameambatana na familia nzima wakiwemo kaka na wadogo zake Mbwana Samatta amesema, hawajawahi kwenda kumpokea Samatta uwanja wa ndege wakiwa kama familia lakini leo waliamua kufanya kitu cha tofauti kwasababu wanahisi hakuna kitu kingine ambacho wanaweza kukifanya kikamfurahisha zaidi ya kwenda uwanja wa ndege kama familia na kumlaki mtoto wao.
Mara baada ya kutua uwanja wa ndege, Samatta alijikuta akishindwa kujizuia kuonsesha furaha aliyokuwanayo baada ya kukutana na familia yake nzima ikiwa inamsubiri uwanjani hapo kwa ajili ya kumpongeza kwa mafanikio yake pamoja na kusalimiana nae.
Mdogowake Samatta akamvalisha taji kakayake kama ishara ya ushindi na pongezi kwa kile mbacho tayari amefanikiwa mpaka sas.
Mashabiki na wadau wa soka nao wakaungana na familia hiyo kumpongeza Samatta ambaye alikuwa ameambata na Thomas Ulimwengu kabla ya kuchukuliwa na viongozi wa TFF na kupelekwa sehemu maalumu ambako watapumzika wakisubiri kuingia kambini kuungana na kikosi kizima cha Stars.
0 comments:
Post a Comment