Tukiizungumzia Bongo Fleva kule ilikotoka kuna majina ambayo huwezi kuyakosa kwenye list, lakini kazi kubwa imefanyika mpaka imefikia hatua kwenye radio na TV kubwa nje ya TZ zimeupokea na kuukubali muziki wetu.
Hongera nyingi kwa kila mtu wa nguvu aliyefanikisha hii safari ikafika pazuri, lakini leo nina kitu tofauti kidogo mtu wa nguvu… tunatambulisha ngoma kali na mpya kila siku, vipi nikikukumbusha kidogo na video za zamani ambazo nyingi zilifanywa hapahapa bongo na zilishika sawasawa miaka hiyo !!
1: Ferooz Feat. Prof Jay– ‘Starehe’… Video ilifanywa na Kampuni ya Benchmark Productions Ltd ambayo inamilikiwa na Madam Rita Paulsen.
2: Mr. Blue– ‘Mapozi’… Kazi ilifanywa na Kampuni ya Wananchi Video Production.
3: Marlaw – ‘Bembeleza’… Kazi ilifanywa na Kampuni ya Blu Framez ya Kenya na Director wa Video ni Tedd Josiah.
4: Bwana Misosi Feat. Hard Mad– ‘Nitoke Vipi?‘.. Hii nayo ilikuwa kazi kali sana ambayo ilifanywa na Kampuni ya Tripod Media.
5: Juma Nature – ‘Hakuna Kulala‘… Yes yes, kali nyingine ndio hii, video ilifanywa na Emptysouls Production.
6: Ali Kiba Feat. Dully Sykes – ‘Kuteseka‘… Katika kazi za kwanza kabisa zilizomtoa Ali Kiba kwenye game hii nayo imo, video ilifanywa na Kampuni ya Wananchi Video.
7: Dully Sykes– ‘Hi‘… Unaambiwa kwenye hit za miaka hiyo, huu mdundo nao umo.
8: Banana Zahir Ally Zorro – ‘Mama Yangu‘… Hii ngoma ilimtambulisha poa sana Banana kwenye Bongo Fleva… Video ilifanywa na Kampuni ya Royal Productions.
9: Q Chief – ‘Si Ulinikataa‘… Video hii pia ilifanywa na Kampuni ya Tripod Media.
10: AY Feat. Mwana FA, Ray C & Banana Zorro– ‘Safi Hiyo‘
0 comments:
Post a Comment