DAUDA TV: ULIPITWA NA MECHI YA AZAM VS SIMBA? ANGALIA MAGOLI YOTE YA AJIB NA BOCCO
December 12, 2015 macho na masikio ya mashabiki wengi wa soka yalielekezwa uwanja wa taifa kwenye mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Simba Sports Club (Dar Derby) mchezo ambao ulimalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa kufungana bao 2-2.
John Bocco ‘Adebayor’ na mshambuliaji wa Simba anaekuja juu Ibrahim Ajib ndio waliibuka mashujaa wa mchezo huo kwa pande zote mbili baada ya kila mmoja kuifungia timu yake bao mbili kwenye mchezo huo.
Bocco alianza kupeleka simanzi Msimbazi kwa goli lake la mapema akizama wavuni dakika ya kwanza ya mchezo baada ya mababeki wa Simba kujichanganya kisha mpira kunaswa na mshambuliaji raia wa Ivory Coast Kipre Tchetche aliyetoa assist kwa Bocco kisha naohodha huyo kumtungua kirahisi golikipa wa Simba Vincent Agban na kuiandikia Azam bao la kuongoza.
Simba wakajibu mapigo kupitia kwa Ajibu aliyezama kambani dakika ya 24 kipindi chakwanza na matokeo hayo kudumu kwa kipindi chote cha kwanza.
Kipindi cha pili Ajib aliingia tena nyavuni kwa Azam na kuipa Simba bao la pili na kuifanya timu yake iongoze mchezo huo kwa goli 2-0 dhidi ya waoka mikate wa Bhakhresa.
Lakini John Bocco akarejesha matumaini ya wana-Azam baada ya kuisawazishia timu yake kwa kufunga goli la pili na kuzifanya timu hizo kugawana pointi moja kila timu.
Dauda TV ‘Timu ya Ushindi’ kama kawaida ilikuwepo uwanjani kuhakikisha unapata kuona kile kilichojiri kwenye mchezo huo japo kwa ufupi ikiwa ni pamoja na kushuhudia magoli yote yalivyofungwa kwenye mchezo huo.galia video ya mchezo wa Azam FC vs Simba SC December 12, 2015.
0 comments:
Post a Comment