Baada
ya beki wa Simba, Ramadhan Kessy, kuutingisha uongozi wa timu hiyo kwa
kutaka kuondoka, kocha wa timu hiyo, Muingereza, Dylan Kerr, amesema
kuwa kama anataka kuondoka na aende tu kwani ameshapatikana mrithi wake.
Mkataba
wa sasa wa Kessy na Simba umebakia miezi sita ambapo anaruhusiwa
kufanya mazungumzo na timu yoyote na amekuwa akisitasita kusaini mkataba
mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.
Kerr
alisema kuwa beki wake Mrundi, Emery Nimubona, ambaye naye anacheza
namba moja na Kessy, ameanza kuonyesha kiwango kizuri, hivyo hana
wasiwasi hata akiondoka.
“Kama
Kessy anataka kuondoka aende tu, kwani hata akiondoka halitakuwa jambo
la kuiumiza sana Simba, kwani kwa sasa beki wetu Emiry (Nimubona)
ameanza kunifurahisha, anacheza vizuri sana tofauti na zamani.
“Leo
(juzi) nimeamua kumuanzisha ili nimuangalie kama kweli atafaa kuziba
pengo la Kessy kama akiondoka na nimeona kweli anaweza, hivyo niwatoe
wasiwasi mashabiki wa Simba, hata akiondoka mrithi wake tunaye,” alisema
Kerr.
0 comments:
Post a Comment