Taarifa za Samatta kujiunga na klabu ya Genk zinasambaa kwa kasi sana na hicho ndiyo kitu ambacho kimefanya mtandao huu umtafute manager wa mchezaji huyo ili aweke wazi baadhi ya mambo ambayo wadau wa soka la Tanzania wamekuwa wakijiuliza kwa muda mrefu juu ya Samatta kwenda kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.
Hapa unaweza kupata majibu ya maswali yote kutoka kwa manager wa Samatta Bw. Jamal Kisongo baada ya kufafanua vitu kwa kina ikiwa ni pamoja na kwanini Samatta anakwenda Ubelgiji na si nchi nyingine za Ulaya sambamba na klabu ambayo atakwenda kuitumikia lakini pia ameweka wazi Samatta amesaini mkataba wa muda gani na Genk.
Ni kweli kwanza kipindi chake cha kikanuni kwa mujibu wa FIFA kwa yeye kuwa na haki ya kusaini kuchagua wapi anataka kwenda na kufanya maamuzi kimefika, kwasababu Mbwana mkataba wake unamalizika April 30, 2016 kwa maana hiyo kwa mujibu wa kanuni ya FIFA, mkataba ukibaki miezi sita na chini ya hapo una haki ya kusaini pre contract na hicho ni kitu cha msingi kabisa.
Kwahiyo kwa hali hii, tafsiri yake ni kwamba, yeye ana haki hiyo na ameitumia nafasi hiyo kwasababu kama zoezi la Mbwana kutaka kuondoka alitaka kuondoka tangu muda mrefu lakini kwasababu Katumbi alikuwa bado anamuhitaji TP Mazembe ikapelekea kuendelea kubaki. Hicho kilikuwa kikwazo kutokana na umuhimu wa kwake yeye ndani ya TP Mazembe.
Kwahiyo ni kipindi ambacho yeye (Katumbi) ametumia nafasi hiyo kuweza kuzungumza na mawakala mbalimbali na kuweza kuafikiana kwamba kijana aende kucheza Ulaya. Ukiondoa January ambapo sasa inabidi akatumikie klabu yake, mkataba wake umebaki miezi mitatu ndani ya TP Mazembe. Miezi hii ndiyo iliyopelekea hii timu ya Genk kuweza kujadiliana na katumbi kuafikiana watamuachia vipi Samatta kama ni bure majira ya joto au aondoke sasa kwa ada flani watayokubaliana.
Sisi kama management tunataka kuona Mbwana Samatta anakua Kisoka, tunaweza tukamuona kwamba Mbwana ni mzuri lakini anaingia katika dunia nyingine ya mpira wa soka, kwa maana hiyo tunataka Mbwana apate mahala penye fursa ya kucheza, mahala ambapo watu watamtegemea, mahala ambapo atafurahia mpira na kujifunza vitu vingi na kuvitumia katika mechi.
Kulikuwa na timu kadhaa, lakini tunasababu za kimsingi pamoja na group la mawakala wetu ambao tulikuwa tunajadiliana nao tuliona kwamba Genk ni timu muafaka kwasababu ya ligi yake. Hatuwezi kumtoa Samatta Afrika na kumpeleka Ulaya moja kwa moja kwenye ligi ngumu, hiyo itakuwa si kwamba kuonesha ushababi kwamba mtoto anaweza kucheza bali inawezekana tukampoteza na sisi hatutaki kumpoteza tunaka apande ngazi afikie mahali pazuri. Tunataka apate uzoefu atambue soka la Ulaya likoje.
Kwahiyo ligi ya Ubelgiji nadhani ni ligi nzuri kwa wachezaji wanaotoka Afrika sawa ligi ya Ufaransa au ligi ya Uholanzi kwasababu siyo kama ligi hizo zenye ushindani mkali na changamoto nyingi kama ligi ya Uingereza, Ujerumani au Italy kwahiyo tumeona Ubelgiji ni sehemu sahihi na kwanini Genk, tumeona Genk tayari wao wenyewe wanamuhitaji kwenye safu yao ya ushambuliaji.
Rais wao anamuhitaji, safu yao ya bodi iliona umuhimu wake lakinia na mwalimu anamuhitaji. Kwahiyo kila mtu ndani ya Genk na Ubelgiji wanamhutaji. Hicho ndicho kitu ambacho tumeona hapo ni mahala sahihi kuliko tungempeleka mahala pengine ambapo walikuwa wanamuhitaji na tumezingatia pia ushauri wa mawakala ambao tunafanya nao kazi.
Kwa maana hiyo tunauhakika kwamba baada ya kushauriana timu ambayo tumeichagua ni timu muafaka ambayo itamjenga Mbwana na baada ya miezi sita au mwaka mmoja anaweza kubadilika na kwenda kwenye timu kubwa na akaweza kuingia kwenye ligi yenye ushindsni zaidi.
Mbwana amesaini mkataba wa miaka miwili ambao atabakiwa na ridhaa ya ku-review na kusaini tena mkataba wa miaka miwili. lakini mkataba wake ni mika miwili hicho ndicho kitu cha kimsingi ambacho kipo.
0 comments:
Post a Comment