Mbwana Samatta (kulia) akiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Mh. Nape Nnauye
Mshambuliaji
wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta leo amekutana na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Mh. Nape Nnauye kwenye ofisi ya
Waziri huyo kwa ajili ya kumuaga kwa niaba ya serikali kabla ya kuelekea
nchini Nigeria kuhudhuria sherehe za ugawaji wa tuzo za wachezaji bora
wa Afrika.
Samatta
amesema anatambua umuhimu wa mchango wa serikali katika kuchangia
mafanikio yake pamoja na soka la Tanzania kwa ujumla na kuongeza kuwa,
endapo atafanikiwa kutwaa tuzo hiyo basi haitakuwa ya kwake binafsi bali
ni ya taifa zima.
Mbwana Samatta akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mh. Nape Nnauye
“Kama
nitafanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika tuzo hiyo haitakuwa
ya kwangu peke yangu bali itakuwa ni ya watanzania wote pamoja na
Tanzania kama nchi”, amesema Samatta ambaye yupo kwenye orodha ya
wachezaji watu ambao wameingia fainali ya kuwania tuzo ya mchezaji bora
Afrika kwa wachezaji wa ligi za Afrika.
“Kabla
ya kwenda sehemu yoyote ile ni lazima upate baraka za wazee ndiyomaana
nimekuja hapa kuaga na kuchota baraka za serikali kwa niaba ya Wiara
inayohusika na michezo kabla ya kuelekea Nigeria kuwania tuzo ya
mchezaji bora Afrika”.
Kwa
upande wa Mh. Nnauye yeye amesema serikali ipo bega kwa bega na Samatta
pamoja na wanamichezo wote huku akimtakia kila laheri mchezaji huyo
katika kinyang’anyiro hicho.
Nnauye
pia amesema serikali inapambana ili kuhakikisha wanamichezo wote
wanafaidika kutokana na kazi zao na itapambana na wale wote ambao
wamekuwa wakila kupitia jasho la wanamichezo.
Samatta na Mh.Nape Nnauye wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari
“Kwa
niaba ya serikali, nakupongeza kwa hatua uliyofikia kwani hadi hapo
umelitangaza vyema taifa letu lakini pia hata tuzo ambayo unawania
endapo utaitwaa itazidi kukutangaza wewe lakini pia nchi yetu
itatangazwa kupitia wewe”, amesema Mh. Nauye.
“Lakini
serikali sasa inasimamia vyema maslahi ya wanamichezo wote ili
wafaidike na kile ambacho wanakitolea jasho na tunataka kupambana na
wale wote ambao wanajinufaisha kupitia jasho la wanamichezo”.
Samatta
pia amempongeza Mh. Nape Nnauye kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge pamoja na
kuteuliwa kuwa waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na
Michezo.
Tuzo
za wachezaji bora Afrika zitatolewa nchini Nigeria January 7, 2016
ambapo Samatta anawania tuzo hiyo ya mcheaji bora Afrika kwa wachezaji
wa ligi za Afrika akiwa pamoja na Bahgdad Bounejah (Etoile du Sahel,
Tunisia) Algeria na Robert Kidiaba (TP Mazembe, Congo DR) Jina la
Samatta limeingia kwenye orodha ya wachezaji watatu wanaowania tuzo hiyo
baada ya kuisaidia timu yake ya TP Mazembe kutwaa kombe la klabu bingwa
Afrika huku yeye akiibuka mfungaji bora wa michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment