Na Ben Shija
MOHAMED
DEWJI Mo bilionea anayetaka kuwekeza bilioni 20 ameupa uongozi wa Simba
hadi keshokutwa Desemba 31 wawe wameamua moja juu ya kukubali au la
mpango wake wa kufanya uwekezaji wa kiasi hicho cha fedha kwa nia ya
kuiendesha klabu hiyo kibiashara.
DEWJI
Mo ameniambia E. sports ya E FM katika mahojiano maalum leo asubuhi
ofisini kwake kuwa anataka viongozi wa Simba chini ya Rais Evans Aveva
waamue moja kama wako tayari Au la na ikifika keshokutwa kama
hawatafanya maamuzi yeye hatoendelea tena na mpango huo na badala yake
ataendelea na biashara zake
MOHAMED
DEWJI Mo anataka kuwekeza kiasi cha sh. Bilioni 20 kunako klabu hiyo
kwa nia ya kuiendesha kibiashara klabu hiyo kongwe kabisa barani Afrika.
Anasema
alikutana na viongozi wa SIMBA Rais Evans AVEVA, akiwa na KASSIM DEWJI
na Musley Ruhwehi ofisni kwake na kuwaeleza dhamira yake hiyo lakini
anaona viongozi hao kama hawako tayari kwa sasa kuona klabu hiyo
inaendeshwa kibiashara kwani mpaka sasa hawajampa jibu la kueleweka.
"KITENGE
nakutuma kawaambie wana Simba kwa ujumla kuwa nimewapa viongozi wao
mpaka Desemba 31 kama hawatafanya maamuzi ya hilo basi nafuta mpango huo
na wasinitafute tena Maana hawatanipata na cm zao sitopokea. Amesema
MOHAMED DEWJI Mo ambaye anatajwa kuwa tajiri zaidi Kijana nchini
Tanzania.
Mo
anasema chini ya uwekezaji atakaofanya atajenga Kiwanja cha Bunju na
kuwa Kiwanja maalum cha mazoezi ya klabu hiyo na pia kama kituo maalum
cha kulea vipaji vya soka kwa vijana ambao baadaye watachezea timu hiyo
ya SIMBA.
Mo
amesema mipango yote hiyo tayari amewaeleza viongozi wa SIMBA chini ya
Rais AVEVA lakini akashangaa mpaka sasa viongozi hao wamekuwa
hawanyooshi maneno na badala yake wanasema bado hawajapata barua rasmi
kutoka kwake.
Anasema
tumeongea hapa ofisini kwangu na viongozi na kuwaeleza ambapo pia
nimewaambia tutaunda bodi ambayo itakuwa na watu saba wanne watatoka
kwake Mo na watatu watatoka upande wao wa uongozi kwa nia ya kuendesha
kibiashara.
Mo
anasema anataka mpango huo uanze haraka iwezekanavyo ikibidi Januari ili
kuanza pia mchakato wa kutuma mascout kusaka wachezaji watakaochezea
Simba baada ya kumalizika kwa Ligi hii inayoendelea.
0 comments:
Post a Comment