Wakati
uongozi wa Simba chini ya Rais Evans Aveva, ukionesha dalili za
kukubaliana na ombi la bilionea, Mohammed Dewji ‘MO’ kuichukua klabu
hiyo kwa ununuzi wa hisa, bodi ya udhamini imekuja juu na kupinga hilo.
MO
ameweka bayana nia yake ya kuwekeza bilioni 20, kwa ajili ya kurejesha
hadhi ya Simba ikiwa haijashiriki michuano ya kimataifa miaka minne
sasa.
Aveva
alikiri kuwepo na mpango wa MO, lakini akasema kuwa suala hilo
linahitaji mchakato mzito mpaka kumfikia maamuzi ya kumpa mamlaka tajiri
huyo.
Alisema
mojawapo na hatua ni kujadili kwa kina thamani ya timu kisha
kulifikisha kwa bodi ya wadhamini kabla ya kuliacha mikononi mwa
wanachama katika mkutano mkuu ili kuridhia uwezekano wa kumuuzia hisa za
umiliki wa timu.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Udhamini, Mzee Hamisi Kilomoni, ametoa rai mapema kuwa
mpango wa kuiachia timu hiyo kutoka mikononi mwa wananchi hauwezekani
kwa hoja yoyote ile.
“Kwanza
tangu Aveva aingie madarakani sijawahi kumuona na hajawahi kuonana na
kiongozi yeyote wa bodi ya udhamini…MO yeye namsikia tu kwenye vyombo
vya habari.
“Hatuko
tayari kuiachia timu kwa vyovyote itakavyokuwa, hatuko tayari kuachia
timu iwe mikononi mwa mtu mmoja kwa ushawishi wa milioni ngapi…kumbuka
hawa wanakuja na kuondoka, sisi tuko palepale na sisi ndiyo wenye hati
ya kufanya hivyo (kuidhinisha).
“Siafiki
uwekezaji unaozungumzwa, si sahihi na haujafuata misingi sahihi,
vinginevyo tutaitelekeza timu kwa ushawishi wa bilioni 20 za mtu,”
alisema mchezaji huyo mwasisi.
Wakati
wengi wakiunga mkono adhima ya MO, kwani timu haina cha kujivunia miaka
80 sasa licha ya kuwa chini ya miliki ya wanachama, Mzee Kilomoni
alifunguka: “Siyo kweli tuliingia Simba haina jengo, leo hii ina majengo
mangapi, uwanja upo lakini wa kulaumiwa ni viongozi wanaongia
madarakani mara kwa mara wanashindwa kuuendeleza siyo kweli kwamba timu
haina kitu.”
0 comments:
Post a Comment