Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma salamu za rambirambi kwa klabu ya Simba SC, kufuatia kifo cha Seleman Said ‘Yeltisn’ kilichotokea jana jijini Dar es salaam.
Katika salamu hizo TFF imesikitishwa na kifo cha kiongozi huyo, ambaye alingoza klabu ya Simba SC na kupelekea kupewa jina la utani la ‘Yelstin” kutokana na ufanisi wake katika kazi na misimamo akifananishwa na aliyekua Rais wa kwanza Urusi wakati huo Boris Yeltsin.
TFF kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini inawapa pole familia ya Seleman Said ‘Yelstin’ ndugu jamaa, marafiki, uongozi na wanachama wa klabu ya Simba kufuatia kifo hicho, na kusema wako pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo.
Mazishi ya marehemu Selaman Said ‘Yelstin’ yanafanyika leo saa 10 kamili jioni katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment