MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

Uchaguzi FIFA: Sifa na Nafasi ya kushinda kwa Wagombea wa FIFA – Mmoja Ajitoa Dakika za Mwisho



Muda mfupi shirikisho la soka duniani FIFa litapata uongozi mpya kwa kuchaguliwa kwa Raisi mpya wa shirikisho hilo.
   Uchaguzi huu umekuja baada ya aliyekuwa Raisi wa shirikisho hilo kujiuzulu kutokana na tuhuma za rushwa – tuhuma ambazo zimekuwa zikiharibi sifa ya shirikisho hilo kwa muda mrefu.
Katika uchaguzi wa leo kutakuwa na wagombea watano ambao wanawania kuchukua madaraka rasmi kutoka kwa Raisi wa Muda wa shirikisho – Issa Hayatou. Wagombea hao ni Sheikh Salman, Prince Ali, Gianni Infantino, Jerome Champagne pamoja na Tokyo Sexwale.
Kuelekea uchaguzi huu – tuangalie wasifu na mambo tofauti ya wagombea pamoja nafasi wanazopewa kupata ushindi.
  1. SHEIKH SALMAN
Umri: 50
Nchi: Bahrain
Kazi: Mkuu wa Shirikisho la soka la Asia
Utabiri: Anapewa nafasi kubwa ya kushinda lakini anapingwa na wanaharakati wa makundi ya haki za binadamu.
Salman alikumbwa na tuhuma ambazo amezikanusha za kuhusika na maandamo ya kisiasa nchini mwako mnamo mwaka 2011, maandamano ambayo yalizusha vurugu kubwa.
Pia ana tuhuma za kuipa Pakistan zawadi ya kocha wa kufundisha timu ya taifa ya nchi hiyo na mwezi mmoja wakampigia Salman kuwa Raisi wa shirikisho la soka la Asia.
Wadau wengi wa soka waliokuwa wanampinga Blatter wanamuona Sheikh Salman atakuwa hana tofauti sana na Blatter ambaye amekuwa na urafiki nae kwa muda mrefu na Salman alimpigania sana Blatter wakati akiandamwa na skendo za ufisadi ndani ya FIFA.
Sheikh Salman anaonya kwamba mpinzani wake Infantino ana mipango ambayo itaifilisi FIFA.
Pia ana sera ya kutaka Kombe la dunia liendelee kuwa na timu 32.
  GIANNI INFANTINO
AGE: 45
COUNTRY: Swiss-Italian
JOB: Katibu Mkuu UEFA

Anapewa nafasi ya pili ya kuibuka na ushindi lakini yeye ni chaguo la pili la nchi za ulaya.
Amegombea tu kwa sababu Raisi wa UEFA Michel Platini amefungiwa.
Tuhuma alizonazo ni mahusiano yake ya dhati na Platini ambaye nae amehusishwa na rushwa na hatimaye kuadhibiwa kifungo cha miaka 6 nje ya soka pia anahusishwa na tuhuma za upangaji matokeo huko Ugiriki.
Ana sera ya mpango wa kutumia nusu ya mapato ya Fifa ya £3.5billion kwa ajili ya maendeleo ya soka.
  PRINCE ALI
AGE: 40
COUNTRY: Jordan
JOB: Aliwahi kuwa mjumbe wa kamati kuu ya FIFA.
Alipata kura nyingi lakini akapoteza dhidi ya Sepp Blatter mnamo May 2015 katika uchaguzi uliopita.
Hata hivyo safari hii hapewi nafasi kubwa kutokana na upinzani wa Sheikh Salman na Infantino ambao wanaungwa mkono na wanachama wengi.
Mwenyewe amekaririwa akisema kwamba mizizi ya FIFA ya zamani bado ipo na uchaguzi wa Raisi utakuwa hivyo hivyo.
  JEROME CHAMPAGNE
AGE: 57
COUNTRY: France
JOB: Mwanadiplomasia na Mtu wa Ndani wa FIFA
Huyu alikuwa mtu wa karibu sana na Blatter – mpambe wa Raisi huyo aliyejiuzulu kwa muda wa miaka 11 lakini wakagombana mnamo mwaka 2010 na akaondoka FIFA.
Hapewi nafasi kubwa ya kushinda kwa sababu hana ufuasi wa wanachama wengi kama ilivyo wapinzani wake japokuwa inaaminika ilani yake ya uongozi imekaa vizuri kuliko wagombea wote – hata hivyo kwa wanaofahamu siasa za FIFA wanasema sera sio kigezo cha kupigiwa kura.
  TOKYO SEXWALE
AGE: 62
COUNTRY: South Africa

– Amejitoa dakika za mwisho kabla ya upigaji kura na labda aliona kabisa kwamba hana nafasi kabisa.
Namna Uchaguzi Unavyofanyika
Kabla ya kupiga kura, kila mgombea anapewa nafasi ya kuzungumza mbele ya wajumbe wa FIFA.
Baada ya hapo wawakilishi wa vyama vyote vya soka duniani 207 wanaingia kwenye sehemu za kupigia kura kwa kufuata mfumo wa alphabet.
Mshindi atahitaji kupata robo tatu ya kura zote au zaidi ili kutangazwa kuwa Raisi mpya.
Ikiwa kura hazitotosha basi kura zinaligwa upya kwenye raundi ya pili na hapo kanuni zinabadilika kidogo – inahitajika wingi kidogo wa kura ili mgombea atangazwe mshindi.
Ikiwa hakuna aliyeshinda kwenye raundi ya pili – mgombea mwenye namba ndogo ya FIFA ataondolewa kwenye kinyang’anyiro na zoezi linaanza upya mpaka mshindi apatikane.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment