MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

KAMA HAKUNA ‘MKUBWA KULIKO SIMBA’, BASI NA UONGOZI HUU UONDOKE MADARAKANI


AVEVA1
Na Ben Shija
Johann Pestalozzi alizaliwa katika mji wa Zurich, Uswisi yapata mwaka 1746. Wazazi wake walikuwa wa asili ya Kiitalia waliohamia Uswisi. Baada ya kufuzu shahada ya sheria katika Chuo Kikuu cha Zuric, Pertalozzi aliamua kuwa mkulima badala ya kufanya kazi aliyosomea.
Baadaye kutokana na matatizo ya kifedha aliyoyapata ilibidi aiache kazi hiyo. Mwaka 1773 alianza kazi ya kuwafundisha watoto maskini kwa kuwaleta nyumbani mwake ili kuwasaidia waondokane na hali mbaya kimaisha iliyokuwa inawakabili.
Alifikiri kuwa kwa kuwaleta nyumbani angeweza kuwasaidia waweze kujiamini na kujisikia kuwa hata wao ni watu kama wengine. Watoto wale walikuwa wakifanya kazi ya kusokota nyuzi za pamba na wakati huohuo alikuwa anawafundisha hesabu na dini.
Kwanza elewa kuwa, elimu ni jumuisho ya maarifa, stadi na mielekeo inayotawaliwa na mila na desturi za jamii. Kwa jumla mtu mwenye elimu ni yule aliye na maarifa, stadi na mielekeo.
Wakati wa jioni walikuwa wanafanya kazi mbalimbbli kama vile kulima bustanini. Wasichana walifundishwa upishi na ushonaji. Mawazo ya Pastolazzi kuhusu elimu yameathiriwa sana na hali ya wakati alioishi. Alipenda sana kuwasaidia wanyonge. Njia nzuri aliyoiona ni kutoa ushauri kuwa elimu ni haki ya kila mtu.
Yasemekana kuwa Pestalozzi alikuwa ni mwanafalsafa wa kwanza kuonesha ubora na ulazima wa kutoa elimu kwa watu wote. Vilevile aliona kuwa elimu ni chombo cha kuinua maisha ya wananchi kwani huwapatia mwanga wa kuweza kujiendeleza wenyewe kukuza stadi zao. Pia aliona elimu kama njia pekee ya kuleta amani na usalama katika ulimwengu.
Nadharia zake nyinyi mwanafalsafa huyo kuwa dhima ya elimu ni kumwandaa anayeipata aweze kukubalika katika jamii yake. Elimu isimtenge mtoto na jamii yake, bali imwezeshe kutambua wajibu na nafasi yake katika jumuiya yake. Pestalozzi pia aliamini kuwa mtoto yeyote huzaliwa akiwa mzuri. Ubaya huanza hapo baadaye.
Kwa hiyo haiba ya mtoto inaweza kujengwa vyema ikiwa mtoto atalelewa katika hali ya upendo. Ukuaji wa mtoto kiakili, na kimwili hutegemea sana upendo. Pestalozzi alisisitiza kuwa elimu ya kazi lazima ianzie nyumbani kwa wazazi kwani hakuna mwalimu yeyote anayeweza kumlea mtoto kama vile mtoto anavyoweza kulelewa na mzazi wake.
Alisisitiza pia kuwa elimu itolewe kwa watoto kwa kuwapa maarifa kulingana na uzoefu, umri, uwezo na mahitaji yao. Vilevile elimu lazima imkomboe na kumpa furaha anayeipata. Ni lazima imsaidie anayeipata kuishi vyema katika jamii yake kwa kutumia maarifa na ujuzi alioupata kutokana na elimu hiyo.
Utambuzi ni jambo la kwanza katika upataji wa elimu au maarifa. Kuona mambo na kuyachunguza ni jambo muhimu na msingi bora wa kujifunza. Katika kutoa elimu, mwanafunzi ndiye lengo muhimu. Elimu itolewe ikizingatiwa kuelewa kwa mwanafunzi kwani kufanya hivyo kutamsaidia katika maisha yake ya baadaye.
Tabia au hali anayokuwa nayo mwalimu inaweza kuathiri maendeleo na tabia ya ujana. Vijana hujifunza kwa njia ya kuiga vitendo na kuchunguza mambo. Iwapo mwalimu atakuwa na mwelekeo mbaya wanafunzi nao watajifunza kuwa na mwelekeo mbaya. Pastalozzi alisisitiza pia kuwa adhabu zisitumike mara kwa mara, kwani zinaweza kupunguza ari ya wanafunzi ya kujinza.
Nimekumbuka mawazo ya Pestalozzi kuhusu elimu kufuatia maendeleo mabaya ya timu ya Simba nje na ndani ya uwanja kwa kipindi cha misimu minne mfululizo sasa. Ikipoteza mchezo wake wa tano msimu (wanne katika uwanja wa Taifa) siku ya Jumapili dhidi ya Mwadui FC, Polisi ilibidi kukusanyika kwa wingi karibu na walipokuwa wamekaa viongozi baadhi wa klabu ya Simba kwa lengo la kuwa-hami na shambulio lolote baya.
Baada ya timu yao kufungwa goli pekee zikiwa zimesalia dakika 17 mchezo kumalizika baadhi ya mashabiki wa Simba walianza kusogea upande walipokuwa viongozi wa klabu yao kwa lengo la moja kwa moja kwenda kuwafanyia fujo kama shinikizo la kuwataka wajiuzulu katika nafasi zao ili kuinusuru timu yao inayozidi kupoteza mwelekeo.
Nimeandika sana kuhusu uongozi huu, nimeeleza sana kuhusu madhaifu ya utawala wa Evance Aveva na mwanzo wa kuanza kuanguka kwa timu hiyo chini ya Ismail Aden Rage mwaka 2012. Leo sina mengi sana zaidi ya kutaka kuwashauri zaidi viongozi wa sasa wa klabu hiyo kujiuzulu wenyewe kama njia ya kujiwajibisha, kinidhamu, kwa kushindwa ili kuwapisha watu wengine kuiongoza klabu hiyo.
Kama viongozi wamechangia kwa kiasi kikubwa kushusha nidhamu ya wachezaji kwa maneno yasiyo na ‘muelekeo’ mara nyingi wanapokuwa katika vyombo vya habari. Ni uongozi uliozuia timu kucheza mfululizo wakati ilipokuwa katika kiwango cha juu eti kwa sababu walikuwa wamecheza game 3 hadi 4 zaidi ya Yanga SC na Azam FC. Kitendo hiki ni sawa na wao wenyewe kuihujumu timu yao kwao ilikuwa ikishinda mfululizo.
Ni uongozi ambao umechangia mlinzi Hassan Kessy kujiunga na Yanga bila hata kuzungumza na Simba ambayo bado ana mkataba nayo. Wamemfungia Kessy kutocheza game tano kwa sababu zisizo za kimpira. Walipunguza morali kwa wachezaji wengine ambao sasa wanaamini ukifanya kosa tu wewe ni adui. Ni kama utawa umejenga chuki kwa wachezaji wanaomaliza mikataba yao na kujaribu kuwaweka katika kundi la ‘kafara ya matokeo mabaya’.
Kauli kuu ya utawala wa Aveva wakati wakifanya maamuzi yao ya kinidhamu ni kwamba, ‘HAKUNA MKUBWA KULIKO KLABU.’ Nafikiri njia yao ya kutoa adhabu mara kwa mara imeleta matokeo mabaya zaidi ndiyo maana hata Ibrahim Ajib alijitengenezea kadi nyekundu ya moja kwa moja tena kwa makusudi kabisa katika game dhidi ya Mwadui.
Kama hakuna ‘MKUBWA KULIKO SIMBA SC BASI NA UONGOZI WA HUU UONDOKE MADARAKANI’ kwa maana wamezidiwa sana.
Wakati Pestalozzi aliamini kuwa walimu wakiandaliwa vizuri wanaweza kufanya kazi nzuri, Simba isitaraji maajabu yoyote ya kimafanikio chini ya utawala wa sasa kwa sababu hawana ufahamu mzuri na mambo ya kandanda.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment