Wiki ijayo atakuwa Las Palmas na kumalizia Malaga (vilabu vya La Liga), hapo ndipo itajulikana mustakabali wa majaribio yake kote huko kwa mujibu wa wakala wake, John Sorzano ambaye anamiliki baadhi ya wachezaji pale EPL akiweno staa wa Crystal Palacr Yannick Bolasie.
Farid aliunganisha moja kwa moja akitokea Tunisia ambako Azam ilienda kucheza mchezo wake wa marudiano wa kombe la shirikisho na kujikuta ikitupwa nje ya mashindano na klabu ya Esperance kwa ushindi wa jumla ya magoli 3-2.
Farid atafanya majaribio hayo na kukaa huko kwa wiki mbili zijazo akitarajiwa kurejea nchini May 19 mwaka huu wakati msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakapokuwa umemalizika.
Mechi pekee ambayo anaweza kuiwahi ni ile ya fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) itakayofanyika May 25 mwaka huu, ambayo Azam FC ilifuzu kwa kuichapa Mwadui FC ya Shinyanga na itacheza dhidi ya Yanga.
0 comments:
Post a Comment