Wachezaji wa Simba Awadh Juma (ushoto) na Ibrahim Ajib (kulia) wakishangilia goli la kwanza lilifungwa na Danny Lyanga
Ushindi wa magoli 2-0 iliyoupata leo timu ya Simba SC dhidi ya Mbeya
City kwenye uwanja wa taifa ni ushindi wa kwanza wa ‘Wekundu hao wa
Msimbazi dhidi ya Mbeya Mbeya City kwenye uwanja wa taifa.
Simba ilikuwa haijawahi kuifunga City kwenye uwanja wa taifa tangu
timu hiyo ilivyopanda kucheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Mechi
ya kwanza Simba ilitoka sare ya kufungana kwa bao 2-2 dhidi ya Mbeya
City kisha ikakubali kichapo cha goli 2-1 kwenye mchezo wa pili kabla ya
leo kuikandamiza kwa mabao 2-0. Kikosi cha Simba kilichoanza dhidi ya Mbeya Citu
Magoli ya Simba kwenye mchezo wa leo yamefungwa na Danny Lyanga
ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa
kiganda Hamisi Kiiza kisha Ibrahim Ajib akatupia bao la pili baada ya
kuongezwa dakika moja zikiwa dakika 90 zimemalizika. Kikosi cha Mbeya City Kilichoanza dhidi ya Simba SCRekodi na matukio muhimu unayotakiwa kujua Simba inafanikiwa kurejea kileleni mwa VPL kwa mara pili msimu huu
Simba inapanda kileleni mwa ligi kwa mara ya pili msimu huu baada ya
kufanya hivyo kwa mara ya kwanza ilipoifunga Stand United kwa bao 2-1
kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga na kufanikiwa kukaa kileleni
kwa mara ya kwanza Febuary 13, 2016 tangu ifanye hivyo misimu mitatu
iliyopita. Beki wa Mbeya City akimzuia winga wa Simba Brian Majwega
Hata hivyo Simba iko mbele kwa mchezo mmoja ikiwa imeshacheza michezo
21 na kufikisha pointi 48 wakati wapinzani wake katika kinyang’anyiro
cha ubingwa Yanga na Azam wao wamecheza mechi 20 wakifanikiwa kukusanya
pointi 47 huku wakiwa na mchezo mmoja wa kiporo kwa kila timu. Ubingwa wa VPL bado mweupe kwa timu tatu za juu
Simba, Yanga na Azam zote zinaweza kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya
Vodacom Tanzania bara msimu huu kutokana na idadi ya pointi ambazo
zinazitofautisha timu hizo pamoja na tofauti ya michezo huku idadi ya
mechi zilizosalia ili ligi kumalizika ikipewa uzito wa wa juu kuamua
nani atatwaa ubingwa msimu huu. Simba imevunja mwiko wa kuteswa na Mbeya City kwenye uwanja wa taifa
Timu hizo tayari zimekutana mara tatu kwenye uwanja wa taifa huku
Simba ikishindwa kutamalaki mara mbili mbele ya City, lakini leo
imefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza wa bao 2-0 na kuzima historia
iliyokuwa imewekwa na wana-Mbeya hao. Beki wa Mbeya City Abubakar Shabani akimdhibiti beki wa Simba Mohamed Hussein Tshabalala
Mbali na kushinda mchezo wa leo, Simba pia iliichapa Mbeya City
kwenye mchezo wa round ya kwanza kwa bao 1-0 kwenye uwanja wa Sokoine
jijini Mbeya hivyo kuchukua pointi zote 6 za msimu huu mbele ya Mbeya
City. Ushindi dhidi ya Mbeya City unamaana gani kwa Simba?
Baada ya kupoteza mechi yao dhidi ya Yanga, Simba inafanikiwa
kushinda mbele ya Mbeya City na kupata matumaini makubwa ya kuwania
ubingwa msimu huu tofauti na endapo wangepoteza mchezo au kutoka sare. Ibrahim Ajib (chini) akijaribu kuchukua mpira nyuma ya mlinzi wa Mbeya City Tumba Sued
Simba sasa wanarejea kwa miguu yote kwenye kinyang’anyiro VPL baada
ya kupunguzwa makali na Yanga walipokubali kichapo cha bao 2-0 na
kuteremshwa kileleni mwa ligi hiyo ambayo bingwa wake ataiwakilisha
Tanzania kwenye michuano ya vilabu bingwa barani Afrika. Nini kinafuata kwa timu hizo baada ya mchezo wa leo?
Simba itakuwa kwenyeji kwenye uwanja wa taifa ikiikaribisha Ndanda FC
ya Mtwara March 10 mwaka huu wakati wakali wa Halmashauri ya jiji la
Mbeya, Mbeya City wenyewe pia wataialika Coastal Union kwenye uwanja wa
Sokoine, Mbeya. Danny Lyanga akimwacha beki wa Simba Tumba Sued
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment