Beki wa kati wa Mwadui FC ya Shinyanga Joram Mgeveke anasema kupata nafasi ya kucheza kwenye klabu ya Simba inategemea na nani amekusajili kwenye timu.
Mgeveke ambaye anamalizia muda wake wa mkopo akiwa na Mwadui anasema, mkataba wake na Simba unamalizika baada ya kumalizika kwa msimu huu.
“Unajua saizi mimi nipo huru sina mkataba na Simba saizi so hata nikirudi kule tunaanza mkataba mpya”, anasema beki huyo ambaye amekuwa nguzo ya kutumainiwa kwenye kikosi cha Julio katika msimu huu.
“Mkuu saizi mimi nimemaliza mkataba na Simba yaani nipo huru kwenda timu yoyote hata kama watataka nirejee kule tutakuwa na maongezi mapya”.
Mgeveke anaendelea kusema kwamba, kucheza na kutokucheza ndani ya klabu ya Simba kunategemea na uongozi wa juu kwasababu wao ndiyo wanafanya usajili, na ili upate nafasi ya kucheza inategemea na kiongozi aliyekusajili ananguvu kiasi gani.
“Dah!!! Unajua timu zile zinakuwa na makundi mengi mkuu kuanzia kwenye uongozi so chanzo kinaanza kule…tatizo kubwa uongozi mwana”, anasema Mgeveke ambaye amecheza mechi zote za ligi isipokuwa mchezo dhidi ya Simba.
Akathibitisha kwamba, wakati yupo Simba utaratibu wa viongozi wa juu kuamua nani acheze ulikuwepo lakini kwasasa hajui nini kinaendelea kwakua hayupo ndani ya klabu hiyo.
Nikamuuliza Mgeveke kama yupo tayari kurejea kwa waajiri wake endapo watataka kumtumia kwa mara nyingine, na akasema kwamba mpira ndiyo ajira yake hivyo atakuwa tayari kama watafikia makubaliano.
“Nipo tayari si unajua hii ndiyo kazi yangu mkali, pia suala la nafasi sina wasiwasi kwa sababu najiamini hata mwaka jana sikupata nafasi pale kutokana na kutoniamini huku kocha kaniamini nafanya kazi ipasavyo hadi saizi huku nimekosa mechi moja ambayo na wao Simba lakini mechi zote nimecheza so najiamini mkali wangu”.
0 comments:
Post a Comment