Mlinda mlango, Juma Kaseja Juma ameamua kuwasilisha barua kwa uongozi wa klabu yake ya Yanga, golikipa huyo wa zamani wa timu ya Simba SC amefikia hatua hiyo baada ya Yanga kushindwa kutekeleza mambo muhimu yaliyomo katika mkataba ambao pande hizo mbili ziliingia, Novemba, 2013. Juma ambaye alikuwa mchezaji huru, alisaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao mara 24 wa zamani kwa makubaliano ya kupewa kiasi cha pesa, Tsh. 40 milioni, malipo ambayo yalipaswa kulipwa kwa awamu mbili.
Kuna wachezaji wachache sana wa nafasi ya golikipa ambao unaweza kuwaweka katika daraja moja na Kaseja. Kwanza ni uwezo wake ambao kwa miaka 13 umemtambulisha kama kipa bora zaidi nchini tangu kuanza kwa karne mpya, pili ni maisha marefu, tatu ni jinsi ambavyo amekuwa akijiandaa kila mwaka kukutana na changamoto mpya na kutopenda kwake anasa. Kaseja amekuwa mfano bora wa kuigwa usio na shaka.
Hawezi kuisha kisoka katika umri wa miaka 29 sasa wakati, Ivo Mapunda ametimiza miaka 35 na bado anacheza kwa kiwango cha juu katika timu ya Simba. Baada ya kuzichezea klabu tatu tu maishani, Kaseja anakwenda wapi?. Siku moja kabla ya Kaseja kuwasilisha barua ya kujiondoa Yanga, mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe alizungumza mbele ya wanahabari kuwa, milango iko wazi kwa Juma kurejea Simba, mahali ambako amecheza kwa miaka 12 kati ya 14 aliyocheza soka la ushindani.
Simba ni nyumbani kwa Kaseja, Yanga ni sehemu ambayo ameitumia kutengeneza pesa tu. Kaseja siku zote hucheza vizuri katika mechi kubwa. Alifanya makosa makubwa katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, Desemba mwaka jana wakati alipoidakia Yanga kwa mara ya kwanza. Yanga ilipoteza mchezo huo baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Simba.
Juma hakuchezeshwa katika mchezo wowote msimu huu katika kikosi cha Yanga. Ubora alionao, Deogratius Munish kwa sasa ndiyo unaomkimbiza, Kaseja. Amekuwa kipa chaguo la pili tangu mchezo dhidi ya Simba. Hakupenda kabisa, licha ya kuonesha uvumilivu na nidhamu hadi meneja wake alipotangaza kuwa, Yanga wanapaswa kumchezesha Kaseja katika kikosi cha kwanza kabla ya kuwavaa, Kagera Sugar.
Marcio Maximo mkufunzi mkuu wa Yanga aliendelea kumtumia, Deo na hata katika mchezo uliopita dhidi ya JKT Mgambo alimpanga, Deo. Yanga walimlipa Kaseja kiasi cha Tsh.20 milioni katika awamu ya kwanza ya malipo ya usajili wake, lakini wameshindwa kumalizia kiasi kilichobaki ( Tsh.20 milioni) katika muda uliokuwa na makubaliano maalumu. Kwa maana hiyo, mwajiri amevunja mwenyewe mkataba kwa kushindwa kutekeleza. Juma ni mchezaji hasa, lakini ni mtu mwenye kufanya mambo yake kwa umakini mkubwa.
Marcio Maximo mkufunzi mkuu wa Yanga aliendelea kumtumia, Deo na hata katika mchezo uliopita dhidi ya JKT Mgambo alimpanga, Deo. Yanga walimlipa Kaseja kiasi cha Tsh.20 milioni katika awamu ya kwanza ya malipo ya usajili wake, lakini wameshindwa kumalizia kiasi kilichobaki ( Tsh.20 milioni) katika muda uliokuwa na makubaliano maalumu. Kwa maana hiyo, mwajiri amevunja mwenyewe mkataba kwa kushindwa kutekeleza. Juma ni mchezaji hasa, lakini ni mtu mwenye kufanya mambo yake kwa umakini mkubwa.
Huyu ndiye mchezaji wa Kitanzania ambaye alifungua usajili wa gharama kubwa nchini. Usajili wa Kaseja kwenda Yanga, 2008 ulimuingizia mchezaji huyo zaidi ya milioni 35, wakati huo mchezaji wa gharama kubwa alikuwa hazidi Tsh.20 milioni. Ndiye mchezaji wa kwanza nchi kulipwa kiasi cha milioni moja kama mshahara wa mwezi huku akipewa nyumba ya kuishi na gari la kutembelea.
Aliporudi Simba baada ya mwaka mmoja alipewa milioni 30. Kaseja aliingiza zaidi ya milioni 80 katika kipindi cha mwaka mmoja na anaweza kuingiza tena milioni Tsh.60 milioni ndani ya mwaka mmoja. Baada ya Yanga kushindwa kutekeleza mambo muhimu yaliyomo katika makubaliano yao, Kaseja amefuata nyayo za Okwi. Yanga hawatekelezi mikataba ya wachezaji wao?. Wachezaji hii ndiyo dawa ya kutetea haki zenu, Alianza Okwi, sasa Juma, wengine zaidi kufuata. Kaseja hakuitaka Yanga mara zote walizomsajili, ila Yanga nao mbona hawakumtumia?
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment