Mshambuliaji Mnigeria, Emeh Godwill Izuchukwu yuko njiani kurejea Simba kama ambavyo blogu hii ilivyoandika wiki iliyopita.
Taarifa za uhakika zimeeleza, suala la kodi kubwa ya nyumba na gharama za maisha ya nchini Norway, zimechangia Mnigeria huyo kurejea Simba.
“Ni kweli, analipwa vizuri angalau, lakini kodi ya nyumba na maisha yako juu sana Norway, hivyo hapati chochote mwisho wa mwaka.
“Nimezungumza na viongozi wa Simba, wamesema wanalijadili lakini kuna asilimia kubwa za kurudi,” kilieleza chanzo.
Izuchukwu sasa anakipiga katika timu ya daraja la pili ya Elverum FC ya nchini Norway.
0 comments:
Post a Comment