Kitendo cha mastaa wengi kujitokeza kutoa misaada mbalimbali kwa watu waliopatwa na majanga ama maafa kimekuwa kikitafsiriwa tofauti, ambapo wapo wanaosema mastaa hao wanafanya hivyo kwa ajili ya kujionyesha mbele za watu, lakini wapo wanaoamini kwamba kitendo hicho huonyesha moyo wa kujitolea kusaidia jamii.
Mastaa wa soka Cristiano Ronaldo, Didier Drogba, Neymaar na Gareth Bale ni baadhi ya mastaa ambao wameingia kwenye kampeni za mapambano dhidi ya Ebola.
Kampeni hiyo imeandaliwa na Shirikisho la Soka Duniani FIFA ambapo kwenye mtandao wa Youtube zimewekwa video zilizopewa jina la “11 Against Ebola” zinazoonyesha mastaa hao wakitoa elimu kwa madaktari na wataalamu wa afya wanaohudumia waathirika wa Ebola Afrika Magharibi namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment