MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

ARGENTINA, URENO ZIMEKUTANA MARA 27, LAKINI LEO ZIMETEKWA NA RONALDO, MESSI

Argentina na Ureno zinakutana leo katika jiji la Manchester, England katika mechi ya kirafiki ambayo ni gumzo zaidi mwaka huu.

Kabla ya hapo, timu hizo zimekutana mara 27 katika mechi za mashindano na zile za kirafiki.
Wachezaji wawili Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ndiyo wameiteka mechi hiyo.
Mambo kadhaa yamefanya wawili hao waifunike mechi hiyo licha ya kuwa ina nyota wengi ambao hata hawatajwi.

Madrid&Barcelona:
Upinzani mkali walionao wawili hao kutokana na ushindani wa timu za katika La Liga, unachangia kwa kiasi kikubwa ushindani huo.

Ballon d'Or:
Ushindani wao katika tuzo ya Ballon d'Or ambayo iko mlangoni, kila mmoja anajua kutakuwa na ushindani mkubwa.

Tusi:
Ronaldo alituhumiwa kumtukana Messi, mwenyewe baadaye akakanusha. Leo itakuwa ni siku ya kwanza wanakutana baada ya tukio hilo.

Mara 26:


Wakali hao wamekutana mara 26, sita kati ya hizo ikiwa ni mechi za fainali na moja kama unaikumbuka ni ile ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Ronaldo akiwa Manchester United na Barcelona ikashinda, ilikuwa mwaka 2009.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment