KIONGERA |
Mshambuliaji Paul ‘Modo’ Kiongera wa Simba, sasa ameingia kwenye mstari mwekundu wa wale ambao wanaweza kuachwa kwenye kikosi hicho.
Simba inafanya kila linalowezekana kupitia dirisha dogo, ili iimarishe kikosi chake.
Kiongera raia wa Kenya aliyeonekana ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao, ameingia kwenye kundi la wanaoweza kutemwa kutokana na kuwa majeruhi.
“Kama atakuwa majeruhi kwa muda mrefu, hakutakuwa na ujanja, ataachwa,” kilieleza chanzo ndani ya Simba.
Simba inahitaji nafasi za kuwaongeza Emeh Izuchukwu anayekipiga nchini Norway na Danny Sserunkuma kutoka Gor Mahia ya Kenya.
Inaonekana kama Kiongera hatakuwa na msaada na Simba na taarifa zinasema, ripoti ya daktari ndiyo itakayoamua.
Uchunguzi wa Championi Jumatano unaonyesha iwapo atatakiwa kupumzika hadi miezi mitano, basi nafasi yake itakwenda kwa Sserunkuma.
Baada ya hapo, bado Simba itaendelea kusaka nafasi ya pili iwapo itakubaliana na Izuchukwu. Hapa ni zamu ya Pierre Kwizera au Amissi Tambwe.
Kitaalamu kunaonekana kuna mkanganyiko, mkataba wa nahodha Joseph Owino unakwisha. Simba wanaendelea kujiuliza kuhusiana na kiwango chake.
Mjadala ni kumuacha Kwizera kwa kuwa akiumia Jonas Mkude itakuwaje? Pia ikiwa kocha mpya atataka ‘holding midfield’ wawili kama ilivyokuwa kwa Zdravko Logarusic, itakuwa vipi? Inachanganya.
Bado swali linakuja kuwa basi aachwe Tambwe! Simba bado wanajiuliza yeye ndiye mfungaji bora msimu uliopita. Utaona bado inachanganya kwao lakini muda utaeleza.
0 comments:
Post a Comment