Kwenye wengi, hakukosi mengi! Kijana mmoja amekuwa kati ya
karibia 600 waliojitokeza kuwania kuichezea timu ya Simba ya vijana chini ya
miaka 20.
Lakini kivutio zaidi ni kwamba kijana huyo, tayari ana pete
ya ndoa ikionyesha ameishaoa na kitambi kuliko hata makocha wawili wa Simba
waliokuwa wanasimamia zoezi hilo.
Yusuf Macho ‘Musso’ na Nico Kiondo ndiyo walikuwa makocha
wanaosimamia zoezi hilo Uwanja wa Mwenge Shooting jijini Dar es Salaam.
Kijana huyo alikuwa kati ya vijana wanaopambana kuhakikisha
wanapata nafasi ya kuichezea Simba B.
Hata hivyo, muonekano wake alianza kuonyesha ni mnyonge na
taratibu alikuwa akijitenga.
Vijana karibu 600 walijitokeza kuwania nafasi ya kuichezea
Simba B na kwa mujibu wa makocha hao, wachezaji 60 ndiyo walikuwa wanatakiwa
katika awamu ya kwanza.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment