Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) itaanza Sept 12 badala ya Agosti 22 ili
kumpa Charles Mkwasa fursa ya kuendelea na program yake kuelekea mechi
ya Taifa Stars dhidi ya Nigeria itakayochezwa Sept 5.
Mechi
ya Ngao ya Jamii (Community Shield) itakayozikutanisha Azam FC dhidi ya
Yanga SC sasa itachezwa Agosti 22 badala ya Agosti 15.
Ratiba
ya Ligi Kuu iliyokuwa imeandaliwa, sasa inafanyiwa marekebisho kwa
ajili ya tarehe mpya ya kuanza, ambapo pamoja na mambo mengine mechi
sasa zitachezwa wikiendi na katikati ya wiki na wikiendi ya Oct 25
hakutakuwa na mechi kupisha Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge.
Klabu za Ligi Kuu zimeandikiwa barua kujulishwa tarehe mpya ya kuanza Ligi, na dirisha la usajili linabaki kama lilivyo.
Wamiliki
wa viwanja vyenye upungufu wameandikiwa barua kutakiwa kurekebisha
upungufu katika muda maalumu, vinginevyo havitaruhusiwa kutumika kwa
ajili ya PL na FDL.
Timu
ya Madini ya Arusha imeruhusiwa kutumia Uwanja wa Nyerere uliopo Mbulu
mkoani Manyara kwa mechi za SDL kwa masharti upungufu uliopo kwenye
uwanja huo urekebishwe kwanza.
0 comments:
Post a Comment