Kwa
mara ya pili, Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, limeiamuru klabu ya
Simba SC kulipa fidia ya kuvunja mkataba na beki wake wa zamani, Mkenya,
Donald Mosoti Omanwa
Simba walivunja mkataba wa Mosoti Agosti 2014 bila matakwa ya mchezaji.
Taarifa
kutoka Kenya zinaeleza kwamba, Simba wanatakiwa kumlipa Mosoti kufikia
Jumatatu ya Julai 27 na wakishindwa kufanya hivyo, keshi hiyo itapelekwa
kamati ya nidhamu ya FIFA.
Simba
walivunja mkataba wa Mosoti akiwa amebakiza mwaka mmoja na miezi mitatu
na kutokana na hali hiyo mlinzi huyo alipeleka kesi FIFA kupitia kwa
mwanasheria wake, Felix Majani.
AMRI YA KULIPA
Baada
ya FIFA kusikiliza pande zote mwezi Februari mwaka huu, waliamuru Simba
imlipe fidia Mosoti ndani ya siku 30 kutoka siku ya maamuzi.
Majaji waliofanya maamuzi hayo ni Thomas
Grimm (Switzerland), Eirik Monsen (Norway) na Zola Majavu (Afrika
kusini) na walisema Simba wakishindwa kulipa hadi siku ya Deadline,
watafikisha kesi kamati ya nidhamu.
Baraza
la Sheria na hadhi za wachezaji la FIFA chini ya kiongozi wake, Sarah
Solemale, limesema kuwa Simba waliandika barua ya kukata rufaa Alhamisi
ya Julai 16 mwaka 2013, lakini haikufuata taratibu, hivyo Desemba 12
mwaka 2013 wakaiamuru imlipe Mosoti fidia ya Dola 13, 800, lakini haijafanya hivyo mpaka leo.
Simba ikikamilisha malipo hayo inatakiwa kupeleka FIFA nakala ya risti ya malipo.
0 comments:
Post a Comment