Baada
ya klabu ya Simba kutangaza nia ya kutaka kumsajili mlinda mlango wa
timu ya Gor Mahia ya Kenya Boniface Oluochi, kipa huyo amesema amesikia
tarifa hizo na yeye yuko tayari kujiunga na wakongwe hao wa soka la
Tanzania na Afrika huku akiweka wazi kuwa anazimia sana kukipiga
Msimbazi na kutoa sabu kadhaa za kuwazimia wakali hao ambao ni wapinzani
wakubwa wa Yanga.
“Kusikia
kweli nimesikia, waongee na timu yangu kama wao watamalizana mimi sina
tatizo. Bado ninamkataba na Gor Mahia wa mwaka mmoja na miezi minne”,
amlisema Oluochi.
Lakini golikipa huyo hakusita kutaja timu anayoizimia alipoulizwa ni timu gani angependa kucheza kati ya Simba na Yanga.
“Mimi
napenda Simba. Kwasabaubu kuna wakenya wengi walishawahi kucheza Simba
na wakafanya vizuri, ndugu yangu Jerry Santo alishawahi kucheza Simba.
Simba ni timu kubwa na inaogopwa”, aliongeza.
Siku
mbili zilizopita mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans
Poppe alitangaza kuwa klabu yao inamuwania mlinda mlango wa Gor Mahia
ambaye pia ni golikipa wa timu ya taifa ya Kenya Boniface Oluochi pamoja
na mshambuliaji wa timu hiyo Michael Olunga.
0 comments:
Post a Comment