Mwanafunzi
wa Uuguzi bi Joyce Torrefranca, ndiye aliyeipiga picha hiyo nje ya
mkahawa huo wa McDonald ulioko katika mki wa Cebu nchini Ufilipino na
akaichapisha kwenye mtandao wake wa kijamii wa Facebook na ujumbe:
''mtoto huyo amenikumbusha niwekee bidii maishani''
Katika picha yake
bi Torrefranca mtoto mwenye umri wa miaka 9,Daniel Cabrera amejikunyata
kwenye kibao anachokitumia kama meza akifanya mabaki ya kazi aliyopewa
shuleni.
Mtoto huyo Cabrera anatumia mwangaza wa bango la kutangaza duka la McDonald kama taa yake akidurusu !
''kwangu mimi kama
mwanafunzi ,nilipigwa na mshangao kutokana na ari ya mwanafunzi huyu
mdogo aliyekuwa amechutama akikamilisha kazi yake ya shuleni bi
Torrefranca aliiambia runinga ya ABS-CBN katika mahojiano.
''kwa hakika ilinipatia changamoto kubwa niendeleee kufanya bidii katika kila jambo linalonikabili''
Muda mchache baada
ya bi Torrefranca kuchapisha picha hiyo kwenye Facebook maelfu ya watu
waliichapisha pia wakisema kuwa ilikuwa imewavutia sana.
''Ukitaka kitu ama
ukitaka kufanikiwa maishani sharti itie bidii katika kila jambo
unalokabiliwa nalo,hivyo utapiga umaskini teke'' alisema bi Torrefranca.
Alipohojiwa kijana huyo Daniel alisema kuwa aligundua babake mzazi alichomwa moto hadi kufa katika ajali mbaya.
Kakake mwengine ni mgonjwa sana alisema Daniel. Kijana
anasema kuwa yeye hulazimika kupiga buku nje ya mkahawa huo wa McDonald
kila usiku akimsubiri mamake akamilishe wajibu wake katika mkahawa
ulioko karibu.
Afisa wa serikali
anayeshughulikia maslahi ya watoto tayari ameitembelea familia ya Daniel
kwa nia ya kuwapa msaada wa kujinasua kutoka kwa minyororo ya
Umaskini. Kwa
upande wake vyombo vya habari vimekuwa vikimmiminia sifa kochokocho bi
Torrefranca kwakuangazia masaibu yanayomkabili kijana daniel.
Chanzo:Kinasaonlinemedia
0 comments:
Post a Comment