AWADHI JUMA AKISHANGILIA NA WENZAKE MARA TU BAADA YA KUCHEKA NA NYAVU... |
Unakumbuka miaka mitatu iliyopita, yote mfululizo Simba
ilikuwa ikipoteza mechi zake katika Simba Day, basi si mwaka huu!
Maana Simba imefuta uteja wa Simba Day ambayo ni siku yake maalum baada ya kuichapa SC Villa ya Uganda kwa bao 1-0.
Katika mechi hiyo tamu kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam, leo, Simba ililazimika kusubiri hadi dakika za jioni kupata bao
hilo kupitia kwa Awadhi Juma aliyeingia kipindi cha pili.
SC Villa nao walionyesha wako vizuri kwa kuipa shida
kubwa Simba ingawa kiungo cha Mwinyi Kazimoto na Said Ndemla kilikuwa
kimepikika.
Kabla ya hapo wachezaji walitambulishwa pamoja na
benchi la ufundi huku kukiwa na mechi mbili za utangulizi ambazo zilikuwa
burudaaani ile mbaya.
HATIMAYE MO DEWJI AMEREJEA UWANJA WA TAIFA TENA... |
UKAWA KAMA KAWA..... |
0 comments:
Post a Comment