Mshambuliaji Laudit Mavugo amesema alikuwa tayari kujiunga Simba kwa moyo safi lakini kutoelewana kwa viongozi wa pande mbili, ndiyo kumesababisha.
Akizungumza na BEN SHIJA, Mavugo amesema kulitokea tofauti ndogo ndogo sana kati ya viongozi wa timu yake ya Vital’O na Simba.
Amesema alishamalizana na Simba kwa maana ya makubaliano, ndiyo maana alichukua hadi baadhi ya fedha lakini waliposhindana wenyewe, hakuwa na ujanja.
“Kitu cha kwanza kilikuwa ni kuhusiana na fedha wanazodai kuhusiana na uhamisho wa Amissi Tambwe ambazo hawajalipwa hadi leo.
“Pili viongozi wa Vital’O waliona Simba kama hawana ushirikiano na wana dharau, hmaana waliwaomba mechi ya kirafiki, hawakujibu wala kujali lolote,” alisema Mavugo.
0 comments:
Post a Comment