Kutokana na maombi na maswali mengi ya wanachama na wapenzi wa Simba, klabu ya Simba ilitafuta njia bora na mbadala ya uuzwaji wa jezi ya kuzifanya zipatikane maeneo mengi zaidi.
Katika kulitekeleza hilo klabu ya Simba iliamua kuanzisha duka la mtandao kupitia www.jumia.co.tz, Tangu uuzaji wa jezi ulipoanza wiki chache zilizopita zaidi ya mashabiki 300 kutoka nje ya Dar es Salaam wameweza kununua jezi na kuweza kuzipata kupitia duka mtandao la Jumia.
Simbasports.co.tz ilipata nafasi yakuongea mwakilishi wa Jumia Tanzania na kusema kuwa “mauzo ya jezi za Simba yanakwenda vizuri sana kwa mikoni tena kuzidi hata matarajio yetu ambavyo tulidhani itakuwa, ni kitu kizuri sasa watu wengi wameanza kuelewa namna ya kupata bidhaa kwa urahisi sana kupitia duka mtandao la Jumia www.jumia.co.tz “.
Klabu ya Simba inaomba wanachama na wapenzi wa Simba kuhakikisha wananunua jezi halali za Simba ili kuongeza mapato katika klabu kwani katika kila jezi Simba inapata faida ya TSH 2,000. Jezi hizo ambazo zinauzwa kwa TSH 15,000 Uongozi wa Simba unaamini hii ni bei rafiki na kila mpenzi na mwanachama wa Simba kuweza kuzinunua. Tunaamini kwamba huu ni mwanzo na siku zijazo mapato ya Simba yataongezeka zaidi.
Ikiwa unahisi jezi ulionunua sio halali tuma ujumbe mfupi kwenye namba hii +255 718 30 26 42 au tutumie ujumbe kwenye barua pepe info@simbasports.co.tz
Simbasports.co.tz inaendelea kuwahamasisha wapenzi na wanachama wa Simba kuweza kuwahi kununua jezi rasmi za Simba kupitia maduka ya UHL Sports yalipo mtaa wa Jamuhuri na Sinza jijini Dar es Salaam pamoja na kwenye duka mtandao la Jumia www.jumia.co.tz
0 comments:
Post a Comment