MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

SIMBA SC WAFIKIRI KWANZA KABLA YA KUAMUA…DIRISHA LINAFUNGWA LEO SAA 5:59 USIKU

UONGOZI wa Simba SC umeripotiwa kuachana na kipa Ivo Mapunda- maana yake itabaki na makipa wawili wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Hao ni Muivory Coast, Vincent Angban na mzalendo Peter Manyika wakati pia kuna kipa aliyepandishwa kutoka timu ya vijana, Dennis Richard.
Msimu uliopita, Manyika alikuwa kama Dennis mbele ya Ivo Mapunda na Hussein Sharrif ‘Casillas’, kipa aliyepandishwa kutoka timu B.
Lakini tofauti ya Manyika na Dennis ni kwamba yeye tayari alianza kukomazwa miaka mitatu iliyopita kwa kuchezea timu za vijana za taifa kuanzia chini ya umri wa miaka 17.
Dennis ni kipa ambaye zaidi ya kudakia Simba B tena kwa kipindi kifupi mno cha msimu uliopita tu, amekuwa akipewa muda mchache katika mechi kadhaa za kirafiki na kikosi cha kwanza tangu Januari mwaka huu.
Ni kipa mzuri, lakini anahitaji kuendelea kukuzwa na kukomazwa taratibu kisoka kabla ya kuanza kupewa majukumu mazito.
Manyika alijkuta anaanza mapema kudakia kikosi cha kwanza cha Simba msimu uliopita, baada ya makipa wote, Ivo na Casillas na kuumia na mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ikawa dhidi ya mahasimu, Yanga SC ambayo alidaka bila kufungwa dakika 90 katika sare ya 0-0.
Tangu hapo, mtoto huyo wa kipa wa zamani wa kimataifa nchini, Manyika Peter aliyewahi kudakia Yanga SC, akaanza kuaminiwa.
Ivo alipona baadaye na kurejea kupokezana na Manyika kudaka, wakati Casillas alimaliza msimu akiwa anauguza ugoko wake ulioumia katika mchezo wa kirafiki Afrika Kusini.
Baada ya msimu, Simba SC ilimuacha Casillas na wiki hii imekaririwa ikisema imemuacha Ivo, huku ikiwa imeripotiwa pia kusajili kipa mmoja tu mpya, Angban.
Dirisha la usajili wa Ligi Kuu linatarajiwa kufungwa Ijumaa maana yake Simba SC wana nafasi ya kusajili tena. Msimu uliopita makipa wawili waliumia na kipa wa tatu, Manyika akaokoa jahazi.
Nimeilezea tofauti ya Manyika na Dennis Richard- maana yake ili  kujidhatiti zaidi kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu, Simba wanapaswa kuwa kipa mwingine mzoefu.
Kama Ivo na Casillas waliumia msimu uliopita, basi lolote linaweza kutokea pia kwa Angban na Manyika- Simba SC wafikirie kwanza kabla ya kuamua kufunga usajili na makipa wawili wazoefu. Siku njema. 

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment