Kocha mkuu wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr amemteua mshambuliaji mkongwe wa klabu hiyo, Musa Hassan Mgosi kuwa nahodha mpya.
Akizungumza
na MPENJA SPORTS mchana huu, kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola
amethibitisha uteuzi huo na kusema kwamba waliokuwa manahodha wa klabu
hiyo, Hassan Isihaka na Jonas Mkude wanatakiwa kuendelea kujifunza kwa
nahodha mpya ambaye ana uzoefu mkubwa.
"Kocha
ameangalia uzoefu, nahodha anatakiwa mtu kama Mgosi, anaweza kuongea na
wachezaji, anahamasisha timu, ndio maana ameteuliwa".
"Timu
inaweza kuwa na manahodha wanne, lakini Isihaka na Mkude wataendelea
kujifunza kwa Mgosi, pindi anapoondoka wataweza kurithi nafasi yake".
Amefafanua Matola.
Kwa upande wake, Mgosi amefurahia uteuzi huo na kuahidi kuunganisha timu.
"Majukumu
yangu ni kuunganisha timu pamoja, kocha ameangalia uzoefu wangu, bila
shaka nitaifanya kazi hiyo ipasavyo". Amesema Mgosi.
0 comments:
Post a Comment