Kikosi cha Simba leo tarehe 3 – 9 – 2015 kinatarajia kuwa na mchezo mwingine wa kirafiki na klabu ya KVZ mchezo utakaofanyika saa 2 usiku katika uwanja wa Amani Zanzibar.
Kikosi cha Simba kilichoweka kambi yake ya mazoezi visiwani Zanzibar chini ya kocha wake mkuu Dylan Kerr pamoja wasaidizi wake kwenye benchi la ufundi, kimetaarifiwa kuwa kipo salama na chenye ari ya ushindi katika msimu mpya ujao wa ligi kuu Tanzania Bara 2015/2016.
“Wachezaji wapo kwenye ari ya juu ya Ushindi na wanafanya mazoezi kwa bidii sana, sisi kama benchi la ufundi tunasema kuwa wapenzi, wanachama na mashabiki wa Simba na soka la Tanzania kwa ujumla wakae tayari kwa ushindani mkubwa utakaooneshwa na kikosi chetu cha Simba”, Alisema Kocha Msaidizi wa Simba Suleiman Matola.
Simbasports.co.tz itakuletea matokeo ya mchezo huu kadri yatakavyokuwa yakipatikana
0 comments:
Post a Comment