SIMBA SC IMEKAMILIKA KUELEEKEA MCHEZO NA MGAMBO, HAJIB WA MABAO NA BEKI LA NGUVU HASSAN ISIHAKA WAMEPIGA MATIZI LEO TANGA
Na Ben Shija, TANGA
WACHEZAJI wawili nyota wa Simba SC, beki Hassan Isihaka (pichani juu) na mshambuliaji Ibrahim Hajib wamefanya mazoezi na timu yao leo mjini hapa kuelekea mchezo wa Jumatano dhidi ya JKT Mgambo.
Wote Hajib na Isihaka walikosa mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji African Sports Jumamosi Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kutokana na kuwa majeruhi.
Lakini kuelekea mchezo wa keshokutwa dhidi ya JKT Mgambo utakaopigwa Mkwakwani pia, Nahodha Msaidizi Isihaka na mshambuliaji tegemeo la mabao, Hajib wamerudi.
Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe ameiambia SIMBA DUME TEMBONI- ONLINE leo kwamba wachezaji wote hao wamefanya mazoezi vizuri kabisa leo kuelekea mchezo wa Jumatano.
“Sasa ni suala la mwalimu mwenyewe kuamua kuwapanga au la, lakini suala la maumivu halipo tena,”amesema Dk Gembe.
Mchezaji pekee aliyebaki majeruhi kati ya waliosafiri na Simba SC Tanga ni beki Samih Hajji Nuhu, wakati viungo Jonas Mkude na Abdi Banda hawakusafiri kabisa na timu.
Kocha Muingereza wa Simba SC, Dyla Kerr ameanza vizuri Ligi Kuu baada ya kuiongoza timu yake kushinda 1-0 dhidi ya Sports Jumamosi Uwanja wa Mkwakwani na keshokutwa atajaribu kutimiza pointi sita katika mechi mbili za mwanzo ugenini.

Ibrahim Hajib (kushoto) naye yuko fiti kuwavaa JKT Mgambo Jumatano |
Mchezaji pekee aliyebaki majeruhi kati ya waliosafiri na Simba SC Tanga ni beki Samih Hajji Nuhu, wakati viungo Jonas Mkude na Abdi Banda hawakusafiri kabisa na timu.
Kocha Muingereza wa Simba SC, Dyla Kerr ameanza vizuri Ligi Kuu baada ya kuiongoza timu yake kushinda 1-0 dhidi ya Sports Jumamosi Uwanja wa Mkwakwani na keshokutwa atajaribu kutimiza pointi sita katika mechi mbili za mwanzo ugenini.
0 comments:
Post a Comment