MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira
Na Karim Boimanda
KATIKA kinachoonekana kuwa ni kukua kwa Demokrasia katika matawi ya klabu ya Simba, tawi jingine la Simba Dume la Temboni nalo limepanga kufanya Uchaguzi mkuu ambao utakuwa ni wiki moja kabla ya ule wa tawi la SDF Tabata.

Akizungumza na BOIPLUS, Mwenyekiti wa tawi hilo, Benny Shija alizitaja nafasi zitakazogombewa katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Disemba 6 kuwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe watano wa kamati ya Utendaji.

"Sisi ni viongozi wa muda tu, sasa tunataka kufanya uchaguzi mkuu ili tupate Mwenyekiti na Makamu wake pamoja na wajumbe watano ambao mmoja ni lazima awe wa kike.

"Zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu lilianza Novemba 18 na litafungwa Novemba 26. Siku inayofuata yaani Novemba 27 itakuwa ni uhakiki wa fomu na 28 Novemba ni maalumu kwa ajili ya mapingamizi kabla wagombea kupitishwa siku ya pili yake. Kampeni zitafanyika kwa siku sita yani Novemba 30 hadi Disemba 5,''alisema Benny



Kwa mujibu wa katiba ya Simba Dume, Mwenyekiti atakayechaguliwa atakuwa na nafasi ya kuteua wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji ambapo mmoja atakuwa mwanaume na mwingine mwanamke.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment