Mbwana Samatta amesema medali yake ya ubingwa wa klabu bingwa Afrika akiwa na klabu yake ya TP Mazembe anai-dedicate kwa babayake mzazi ambaye ni mtu muhimu kwenye maisha yake huku akisema anatamani kama mamayake angekuwepo ili ashuhudie mafanikio yake aliyoyapata.
Licha ya kuibuka mfungaji bora, Samatta amesema alikuwa anatamani zaidi kuchukua ubingwa wa mashindano hayo kuliko kutwaa kiatu cha mfungaji bora.
“Nimemaliza nikiwa mfungaji bora lakini kitu nilichokuwa nakitamani sana ni kutwaa ubingwa, nilikuwa nahamu nao zaidi na hii imekuwa historia kwangu”, amesema Samatta.
“Nai-dedicate medali hii kwa babayangu kwa jinsi ninavyompenda na kumuheshimu kwasababu amenilea mpaka nimefika hapa, nampa huu ushindi, nadhani ingekua vizuri kama mamayangu angekuwepo leo na kushuhudia mafanikio yangu, lakini bahati mbaya ameshafariki siku nyingi kwahiyo nimebakiwa na mzee pekeyake”.
Samatta amechukua tuzo ya mfungaji bora wa michuano ya vilabu bingwa Afrika baada ya kufunga jumla ya magoli nane na kumpiku mpinzani wake Bakry ‘Al Medina’ Babiker wa Al Merreikh.
0 comments:
Post a Comment