Nyota wa Tanzania anaecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Thomas Ulimwengu amesema, inawezekana kwa wachezaji wa Tanzania kutoka na kufika mbali zaidi kwenye soka bila kupita kwenye vilabu vikongwe nchini vya Simba na Yanga.
Ulimwengu hajawahi kuvitumikia vilabu hivyo vikongwe hapa nchini kabla ya kwenda Mazembe tofauti na nyota wengi wa Tanzania ambao hujenga majina yao kupitia kwenye vilabu hivyo vyenye historia kubwa kwenye soka la Tanzania.
Lakini Ulimwengu hakusita kuonesha furaha yake baada ya kuisaidia timu yake ya TP Mazembe kutwaa taji la klabu bingwa Afrika kwa mara ya tano.
“Ninafuraha sana nimetimiza ndoto zangu nilizokuwa nikiziota sikunyingi za kuchukua ubingwa wa Afrika nikiwa na TP Mazembe. Hapa bado sio mwisho mambo mazuri yanakuja, nataka kusonga mbele zaidi ya hapa” aliesema Ulimwengu akiwa mwenye furaha kubwa.
“Inawezekana kufika huku bila kupita Simba na Yanga kama utajitolea na kupambana kutimiza ndoto na malengo uliyojiwekea”.
Wachezaji wengi wa Tanzania wamekuwa na ndoto za kucheza Simba na Yanga wakiamini ni mahala sahihi kabla ya kutoka kwenda kucheza soka nje ya nchi kitu ambacho Ulimwengu anasema haoni kama kuna ukweli ndani ya hilo huku yeye akisisitiza kujituma na kusimamia malengo ndiko kunaweza kukupa mafanikio bila kujali upo wapi.
0 comments:
Post a Comment